TAMADUNI NA SHERIA KANDAMIZI KATIKA TAMTHILIA YA JENEZA KUTOKA SAURABIA (2025)
Keywords:
Miiko, sheria, tamaduni, ukandamizaji, Saurabia.Abstract
Utafiti huu unachunguza namna tamaduni na sheria kandamizi zinavyojitokeza katika Tamthilia ya Jeneza Kutoka Saurabia. Lengo kuu ni kufichua tamaduni na sheria kandamizi na athari zake kwa maisha ya wahusika. Licha ya kuwa tamaduni na sheria huwasilishwa kama mihimili ya utaratibu na maadili katika jamii, zinaweza kutumiwa kama nyenzo za ukandamizaji na unyanyasaji. Fasihi inachukuliwa kama chombo muhimu kinachoweza kufumbua macho ya jamii kwa kufichua ukweli uliojificha nyuma ya mila na taratibu zinazoonekana kuwa za kawaida. Ni kwa msingi huu ambapo utafiti huu unafanya uchambuzi wa kina kuhusu mwingiliano kati ya tamaduni na sheria kama mihimili miwili inayoweza kushirikiana kuendeleza ukandamizaji katika tamthilia ya Jeneza Kutoka Saurabia. Utafiti huu unaongozwa na Nadharia ya Uhakiki wa Kijamii iliyoasisiwa na Marx na Engels (1848) ambayo inatoa mwanga angavu katika kuchambua masuala ya mamlaka, itikadi na upinzani wa wahusika dhidi ya mifumo dhalimu, na hivyo kuwezesha uelewa wa kina wa namna jamii inavyounda na kuhalalisha sheria zinazoweza kuathiri uhuru wa mtu binafsi. Utafiti huu umefanyika maktabani. Data imekusanywa kwa njia ya usomaji wa kina na uchambuzi wa suala la utamaduni na sheria kandamizi katika tamthilia teule. Sampuli lengwa ni tamthilia ya Jeneza kutoka Saurabia ambayo inasheheni masuala ibuka ya tamaduni na sheria kandamizi. Mbinu ya usampulishaji ambayo imetumika ni mbinu kusudio. Data iliyopatikana katika tamthilia teule imechanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti ambayo ni kuchunguza tamaduni na sheria kandamizi katika tamthilia ya Jeneza kutoka Saurabia. Data iliyokusanywa na kuchanganuliwa imewasilishwa kwa njia ya maelezo na utoaji mifano. Matokeo yanaonyesha kuwa tamaduni na sheria kandamizi hutumika kama zana za kudhibiti na kunyima wahusika haki zao za msingi. Masuala ya tamaduni na sheria kandamizi yanadhihirika katika misingi ya kijinsia na kimadaraka, huku yakizua migogoro katika jamii. Hata hivyo, uwepo wa sauti za upinzani unaashiria mwamko na uwezekano wa mageuzi. Utafiti unapendekeza haja ya jamii kufanya tathmini upya ya mila na sheria zisizozingatia haki za binadamu. Isitoshe, makala hii inahimiza tafiti zaidi za kifasihi linganishi, ili kupanua upeo wa uelewa kuhusu mchango wa fasihi katika kupinga ukandamizaji na kuchochea mabadiliko chanya ya kijamii. Kwa jumla tamthilia ya Jeneza kutoka Saurabia inajadili masuala ibuka ambayo yamejumuishwa katika suala la Maendeleo Endelevu. Baadhi ya malengo ya maendeleo endelevu ni usawa wa kijinsia, afya, elimu bora na mengineyo ambayo mwandishi anaonyesha vile malengo haya yamepuuzwa kiasi cha kufanya mabinti kwenda kutafuta kazi ughaibuni ili kukidhi malengo hayo katika familia zao, jambo ambalo husababisha maafa na kurudishwa wakiwa wafu kwenye jeneza.
References
Bhabha, H. (1994). The Location of Culture. London: Routledge.
Durkheim, E. (2013). Durkheim and the Law. Palgrave Macmillan
Eagleton, T. (2002). Marxism and Lliterary Ccriticism. Routledge
Essel, E. (2018). “The Role of Taboos in African Governance System”. In Econimic and Social journal
Geertz, C. (2017). The Interpretation of Cultures. USA: Basic Books
Kombo, D. & Trump, D. (2006). Proposal and thesis writing: An introduction. Nairobi: Parlines Publication Africa.
Lune, H. (2010). Perspectives in social research methods and analysis. Thousand Oaks: Sage Publication Inc.
Malinowski (2014). A Scientific Theory of Culture and other Essays. Routledge.
Marx, K. (2021). The Research Handbook on Law and Marxism. Edward Elgar Publishing.
Mbaabu, I. (1985). Swahili Culture and Society. Nairobi: Kenya Publishing & Book Marketing
Mbatiah, M. (2018). Fasihi na jamii. Nairobi: Longhorn.
Mberia, K. (2025). Jeneza Kutoka Saurabia. Nairobi: Marimba publishers Limited.
Pound, R. (2012). Jurisprudence. USA: LawBooks Exchange Ltd.
Ritchie, J. & Lewis, J. (2003). Qualitative research practice: A guide for social sciences students and researchers. London: Sage Publications.
Tylor, E.B. (2024). Primitive Culture Research into the Development of Mythiology Philosophy and Religion, Art and Custom. London: Dover Publication.
Vygotsky, L. (1986). Thought and Language. MIT Press.
United General Assembly (2015) Transforming our world: The 2030 Agenda For Sustainable Development. (Resolution A/RES/70/1. United Nations
Wafula, R. M. & Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Jomo Kenyatta Foundation.
Wamitila, K. W. (2003). Msingi cha uchambuzi wa fasihi. Nairobi: Vide-Muwa
Publishers.
Weber, M. (1954). Max Weber on Law in Economy and Society. USA. Harvard University Press.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 International Research Journal of Rongo University

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.
Creative Commons (CC) BY Attribution
Copyright © 2025 Rongo University. All Rights Reserved